KUNENA KWA LUGHA

on Aug 5, 2012

Karibu ndugu msomaji ulietembelea Blogu hii, leo ningependa utambue zawadi kuu aliyokupatia mweyezi Mungu ambayo ni uhai ulionao, wengi wangependa sana kufika siku ya leo lakini hawakuweza. Sasa basi ni vyema tukatambua kuwa pamoja na kazi ngumu ya kutafuta liziki ya kila siku pia tusisahau kuutafuta ufalme wake baba MUNGU aliye mkuu. Katika dunia hii utaona ama pengine kusikia watu wakisema “KUNENA KWA LUGHA” Hebu tujiulize maswali yafuatayo huku tukiangalia maadiko yanasemaje juu ya hayo:-
1)Siki ya pentekoste neno gani lililotukia kwa mitume wa kanisa la kwanza? “kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote wakawa wameketi……….wote wakajazwa roho mtakatifu.” Mdo. 2:2-4
2)Baada ya kujazwa Roho mtakatifu mitume walisema jinsi gani? “wakaanza kusemakwa lugha nyingine, kama roho alivyowajalia kutamka” Fungu la 4
3)Karamaza Roho zimetolewa kwa kusudi gani? “kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.” Efe. 4:12
4)Karama ya lugha imekusudiwa kwa ajili ya nani? “Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini.” 1 Kor 14:22
5)Wanafunzi wengine walipokuwa wanaleta machafuko kanisani kwa kujifanya kunena kwa lugha ngeni Paulo alitoa mafundisho gani? “Ila sasa, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini?” 1 Kor. 14: 6
“VIvyona ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje?” Maana mtakuwa mkinena hewani tu.” Fungu la 9.
“Lakini katika kanisa napenda kunena mameno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, napenda kunena maneno matano kwa akili zangu nipate kuwafundisha engine, zaidi ya kunena maneno kumi elfukwa ligha.” Fungu la 19.
“Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha kasha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, Je! Hawatasema kwamba mna wazimu?” Fungu la 23.
“Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja afasiri” Fungu la 27.
“Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa, aseme na nafsi yake tena na MUNGU.” Fungu la 28.
6)Kwa nini Paulo alitoa mafundisho hayo ya uangalifu juu ya jambo la kunena kwa lugha? Kwa sababu kanisa si mahali Pa kufanya makelele ama machafuko. “Kwa maana MUNGU si MUNGU wa machafuko, bali wa amani, vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.” Fungu la 33
7)Paulo asema ya kwamaba mwisho wa maneno haya ni nini? “kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.” Mafungu 39,40 8)Karama za Roho zimagawanywa jinsi gani? “Lakini kazi hizi huzitenda Roho huyo mmoja, yeye Yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.” 1 Kor. 12:11.
9)Karama ya lugha itatolewa kwa kila aaminiye? “Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wotw wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha?” Mafungu 29,30.
10)Katika yote tufanyayo kusudi letu lingekuwa nini? “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa MUNGU.” 1 Kor. 10:31
TAFAKARI: Makelele au machafuko hayawezi kumtukuza MUNGU. Twaweza kutazamia ya kwamba Shetani atatafuta alete machafuko katika kanisa la MUNGU kwa kuzifananisha karama za Roho. Iliyoonekana zaidi ya nyingine za karama hizo za Uongo ni ile karama ya kunena kwa lugha. Twapaswa kuyasoma maandiko na kuyatafakari kwa kina. Nawatakia jumapili njema na Mungu awabariki, pia nakushauri tembelea Blogu hii kila jumapili ili tujifunze walau kitu kimoja tu katika maandiko baada ya kazi ngumu ya wiki nzima ya mahangaiko ya kutafuta mkate wa kila siku
Sponsered By Jacob Mwaipopo
www.pox10.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment